WOMEN JUST NEVER KNOW WHAT THEIR PARTNERS ARE BRINGING BACK HOME.

I Would Like To Advise Men In Our Society To Stick To One  Partner. 
Hi sporah!
Mungu amekuwa mwema kwako na kwangu pia sifa kwake. Ni kuhusu yale uliyotaka tuishirikishe jamii pengine yaweza kuelimika.

Mie niliishi na mwanaume fulani ambaye hatukufunga ndoa ila tuliishi tu na kubahatika kupata mtoto mmoja wa kike (Maurine). Mwanzo wa mahusiano yatu kama ujuavyo ilikuwa ni amani na furaha pia, lakini baada tu ya kubeba mimba nakumbuka kipindi cha mwanzo niliteseka sana kutapika sana so nikawa sili na nilikonda vibaya mno hadi wakati fulani tulikuwa na huyo mwenzangu mjini akawa hataki kutembea na mie yaani kama ananikwepa kwepa vile. nilinotisi huko kutengwa nikajisikia vibaya sana then baadaye nikamuuliza akasema eti nimekonda sana natisha. Tukaendelea hadi nikajifungua mwanaume ni wa kurudi usiku nyumbani hampangi kitu kikapangika. Baada ya kutoka uzazi eti anasema "mh mke wangu umenenepa hipsi zimerudi mahali yake sasa" nikajua kumbe mwenzangu anapenda tu mwili wangu na sio mapenzi ya dhati. Tuliendelea hivyo dadangu mambo yakageuka anataka mtoto tu anasema hata nikiondoka hajali mradi nIlishampatia mtoto. (nimepiga picha naye kwa profile yangu). Mahusiano nje ndo ilikuwa balaa leo atavunja cmu na line na kuomba msamaha lakinI baada ya muda amerudia hilo hilo.

mwisho pengine nikaona ngoja tuhamie jirani na kwao pengine atakuwa na adabu kwa wazazi wake. Dada yangu! ndo niliharibu! familia ya kwao ni ile ya kusikiliza mtoto wao mie nikawa ndo msumari kwao. Sikupata ushirikiano kwa wazazi baba mkwe kidogo alikuwa upande wangu lakini watoto wote walikuwa upande wa mama so wakiamua jambo inabidi tu baba akubaliane nalo. ilifika hatua hadi huyo mwanaume anawasiliana na wanawake bila woga, kutumiana messege, na kuna kipindi nilimwonyesha wifi yangu messege kuona jinsi kaka yao alivyokuwa ananitenda waliishia tu kusema "jamani kwanini anafanya hivyo" bila msaada wowote.mwisho niliona tu yamenishinda maana sometimes haji nyumbani na akija ni matatizo tu nyumbani. Nikaamua kuondoka tatizo kwao walikuwa wanataka mtoto so wakati nimeondoka dada yangu tulinyang'anyana mtoto wangu niliyemzaa kama twagombea mpira. she was 21/2yrs old. Niliteseka sana that day cose ni mengi sana yalitokea nashindwa hata kuyaandika maana huwa naumia sana, nililia sana mwisho nikaondoka na mtoto cose alikuwa amenizoea sana. nilikaa naye kama miezi 4 wakaja kuninyang'anya mtoto wangu Sporah mimi ni mpole na walifanya hivyo wakijua sitawaweza maana wana pesa na familia yetu ni ya hali ya kawaida sana. sijui ni jinsi gani unaona maumivu ambayo nilijikuta nimeyabeba hadi leo nikikumbuka machozi hayaachi kutoka. kuona binadamu anaweza kuwa mbaya kuliko hata simba. Mwanzoni huyo kijana hakutaka hata nikamsalimie mtoto lakini nilienda kwa nguvu kumsalimia na nilikuwa nikifika ni kilio tu kwa mtoto wangu na mimi mwenyewe na jinsi sometimes nilivyokuwa namkuta nilikuwa naumia sana kuna cares kama kumwogesha, kumbembeleza na mambo mengi alikuwa anakosa sa ikifika wakati wa mie kuondoka na kumwacha ilikuwa ngumu sana. Nilijaribu kwenda chama fulani cha sheria mwanzoni walinisikiliza ila mwishoni ikawa kama wamepewa rushwa ikawa ni kupigwa tarehe tuu bila msaada wowote, ndipo nilipopata rafiki akanipeleka upande wa pili wa Mungu. Hapo nimepata pumziko, mimi nilitamani kujiua baada ya kunyang'anywa mtoto lakini ashukuriwe huyu Mungu wa Mbinguni aliyeniokoa na kuniona wa thamani. Glory be to God Almighty.


Hadi navyoandika huu ujumbe mtoto bado yupo kwa bibi na babu mzaa baba yake ila ujue sporah haikuwa rahisi kama ninavyoandika hivi leo kuishi bila mtoto uliyemzoea ilikuwa  ni ngumu sana kwangu naishi tu kwa imani basi wamekataa kunipa lakini ninamwamini huyu Mungu wa Mbinguni kuwa mtoto tayari Bwana Yesu ameshatengeneza njia ya yeye kurudi kwa mama yake bila kushindana na binadamu, maana Mungu anasema "vita si vyetu ni vya kwake hivyo tumwachiye yeye". Haleluya.

USHAURI:

Nilitamani hata kuwapa hawa waigizaji hili jambo maana sijawahi ona kwa filamu juu ya hizi familia tajiri jinsi zinavyonyanyasa wake ama waume na watoto wao eti kisa upande wa pili hawana pesa. hili jambo limenitesa na limekuwa challenge kwangu kwa kuendelea kuimarisha uchumi wa kwetu ili wadogo zangu wasiteseke kama mie ni wengi sana sporah wapo kwenye maisha kama hayo na wanateseka sana.

Pili.

Napenda uwe unatoa ushahuri kwa wanaume wajitahid kuwa na mpenzi mmoja, inaumiza kumtenda mkeo namna hiyo ilihali yeye ndio anakufanyia kila kitu bila hata kulalamika. mimi nina imani kuwa mwanaume akibadilika am telling you NDOA ZITAKUWA PARADISO. Ni kitu ambacho nilishakifanyia uchunguzi na kuuliza kabisa baadhi yao (wanaume) ndo hapo inafikia wengi (wanawake) wanatamani kuolewa na watu wa nje wakiamini kuwa wametulia. mfano mie niliamua kuwa its beta niolewe na mtu ambaye ameadopt lifestye ya ulaya nikiamini kuwa wazungu hawana uwongo mwingi kwenye mapenzi kam watanzania akiamua kuwa na mwingine anakuambia live na mnaachana kwa amani. Lakini hapa dadangu ni taabu mnakuwa mmepangwa hata sita na kama wote ni warahisi atatembea nao wote. Mungu atuhurumie.

Mwisho kabisa nashukuru kwa kuchukua muda wako na kusoma huu ujumbe for real natamani hata kuhojiwa na media yoyote ingekuwa rahisi kuadvice na kueleza kwa kifupi zaidi na watu wakaelewa vizuri zaidi. Mungu wangu wa Minguni akubariki Sporah uzidi kushine.
 ushare na mie huu hii mistari (1John 4:4, Isaiah 60 yote) kwani imekuwa baraka sana katika maisha yangu haya ya upweke. Mungu amekuwa akinitia moyo na hii mistari sana. na kwako iwe hivo hivo. Much love from  Anansia Uronu.


ENGLISH VERSION
Hi Sporah!
I praise God for all He has done for me and everyone.
I had a life-partner, We weren’t married, just stayed together, and we were Blessed with a beautiful baby girl (Maureen).
Our relationship was ‘’as it normally is’’ Perfect in the beginning. But things became different when I got pregnant; where I fell sick all the time, couldn’t eat so lost a lot of weight; got to a point my partner would avoid being seen with me in Public; he said I was too skinny and unappealing to walk with him.
I really thought things will change after I give birth; but boy was I wrong. He continuously came home late and nothing we tried to plan came to life. After I gave birth, my body was back to normal and he smiled a bit more; which worried me that probably my body was the only thing he liked about me, and maybe we don’t share the same kind of Love and passion towards each other. This was confirmed to me, when he mentioned that the only factor of our relationship after birth was the child, that I was non-relevant to him, and that it wouldn’t really bother him if I left, as long as I left the child behind. I ignored all that, but things got worse when I would find messages in his phone and all sorts from other women.


So I thought maybe it would be a good idea to move closer to his parents, maybe he would be respectful to his family, at least enough to respect our relationship too; only to find out that his family only took his word, and I became the enemy. My father in law was the only one on my side but somehow pushed by the rest of the family against me and so had no support. It got to a point that my partner will contact other women without hiding it from me, he just didn’t care. I showed my sister in law the messages from other women in his phone, but all she said was she didn’t understand why her brother did this, and that was it.
I decided to leave coz it got too much for me, when he wouldn’t come back home at times, even worse when he did; coz he made sure I didn’t have peace in the house. It’s unreal and truly sad how the family fought to take my child away from me when they were told I was moving out. It’s very painful, even to think about now, as I write to you Sporah. I was able to leave with my child. I stayed with her for 4months and the family came and took her away from me. They did this because they knew they could; their family was rich and mine wasn’t.
I will never understand how a human being can be so spiteful. It hurts to know that I was in Love with someone who did his best to harm me.
At first he wouldn’t let me even visit my own child, after they took her away; but I was later able to.
It was hard for me to see my child in a situation where she wasn’t even receiving the basic care without me; even as simple as bathing him. Having to leave him there after my visit, was an everyday battle for me. I decided to take matters to higher places and contacted the law authority; they wanted to be helpful but later dismissed my case; I could tell they were bribed by my partner’s family. That’s when I met a friend who advised me to get closer to God instead; and since then, I have been peaceful after attempting to kill myself. With everything that had happened to me, I’m Blessed to still be sane, and I thank God everyday for that. Glory be to God Almighty.


Up to this day, the child is still with my Ex-partner’s parents and it’s hard and painful to me but I know God will keep me strong. I live by faith, that one day my Lord Jesus will make a way for my child to be brought back to me without me having to fight with human beings anymore. As the Bible says that our battles are not ours to fight, but His, so I leave everything to God, to take care of. Amen.


I thought of giving my story to the Tanzanian film industry, so those going through the same situation, could be encouraged and made strong. Also so people can see how those in relationships with those from the more fortunate backgrounds, can be as mistreated as I was. How wealth becomes more important than Love and care. This has been a challenging part of my life and I wouldn’t wish it to any other person; and I hope others are empowered and encouraged despite their background from knowing my story.


I would also like to advise the men in our society to stick to one partner. It’s painful for the women, who happily do everything for you but also having to deal with the hurt you bring to her. I believe, once a man loves and cares for his woman, and his woman alone; marriage will be the paradise has it was created to be in the first place. Without all the heartache and most of all, diseases in the world, Women just never know what their partners are bringing back home. God feel sorry for Us and save Us please.


Lastly, I thank you for taking time to read my story. I hope I get more opportunities to inspire and encourage others, as you gave me a chance to do today. May the Lord continue to Bless you Sporah.
I would please like to share these encouraging Bible passages (1John 4:4, Isaiah 60); as these verses motivated me to get back on my feet and feel worthy again. I hope they Bless others, as did me.
Much Love and All the Blessings.
From Anansia Uronu.

Story Translated by:
Linda Lynn Kapinga
Fredy Mtoi
  

DO YOU HAVE YOUR OWN TOUCHING AND INSPIRING STORY TO TELL?
LOVE STORY, VIOLENCE, SEXUAL ABUSE, OR ANY DISASTER STORIES? HAVE YOU EVER GIVE UP ON YOUR DREAMS AND REGRET IT? OR PURSUE YOUR DREAMS AND IT SUCCEEDED? WE WANT TO HEAR YOUR STORIES AND INSPIRE MORE MUCH PEOPLE WITH YOUR STORIES! YOUR STORY MIGHT HELP ANOTHER PERSON IN OVERCOMING CHALLENGES.
Email: sporahtvshow@gmail.com
Tel: 02075360382. 
Mob: 07932911205

12 comments:

 1. Anonymous08:08

  pole sana dada

  ReplyDelete
 2. Anonymous09:09

  MEEEENNNN...!

  ReplyDelete
 3. Anonymous09:19

  You have a very beautiful girl, very pretty. And Your very lucky young lady because you know GOD.
  I'm thinking about something that a lover once told me. They said that if your past relationship nearly killed you, then you shouldn't be so quick to jump in another one. Perhaps, you should wait. That would probably be the best thing to do, because you could do the slightest thing to remind them of that certain person. Stay strong and Remember This, YOUR DOUGHTIER WILL ALWAYS BE YOURS.

  ReplyDelete
 4. Anonymous09:47

  It's amazing to me how all the "nice girls" seem to get bad guys! You definitely seem like a nice girl. I am a 31 year old single woman, and I've been through lots of relationship stuff. Here is my advice to you:
  >Take care of yourself. Always strive to be the best you can be and to make your life a good one for YOU. Happy people are attractive and make good partners.
  >Hope for everything, but EXPECT NOTHING. Don't put your life on hold waiting for him to see what you want him to.
  >Don't stop caring. (Especially to your daughter and Even to his family) There is nothing wrong with truly caring about someone.

  ReplyDelete
 5. Anonymous09:51

  I have been in a similar situation recently, you should not give up on your daughter my dear, Let his family know that you care about your daughter. And she is your bloood for G sake.

  ReplyDelete
 6. Anonymous17:03

  huyo hakukupenda kabisaaa dada, we msahau tu.
  Pole sana.

  ReplyDelete
 7. Anonymous18:27

  Sikuizi matajiri wanaona matajiri wenzao dada, hapo ilikua tu bahati mbaya, ila you know what.!!
  Your so beautiful and very intelligent, thats all matter.

  ReplyDelete
 8. Anonymous02:17

  Stay beautiful SKY IS THE LIMIT.

  ReplyDelete
 9. Anonymous04:34

  I think she need to maintain her body the way she used to.

  ReplyDelete
 10. Anonymous02:03

  Wewe ni mzuri sana sana dada, huyo mwanaume sikutishie, utapata mwanaume mzuri tu na atakaekupenda kwa dhati, Endelea kusali na mkabithi yote Muumba, hakuna linaloshindikana kwake.

  ReplyDelete
 11. Anonymous11:40

  thank you so much guys for your beautiful message. am very blessed for your encouragement. Bless you.

  ReplyDelete
 12. Anansia11:50

  napenda kuigiza jamani naombeni mniconect na bongo movie yeyote. hii message ingefika vizuri (kwa urahisi)sana kwa jamii.

  ReplyDelete